M.A.A., 28, a school teacher in Nairobi, Kenya

Mimi ni mwalimu wa shule ya kidato cha pili iliyoko magharibi mwa Kenya. Ninasomesha wanafunzi wa kidato cha kwanza,cha pili, cha tatu hadi ya kidato cha nne. Nina takriban wanafunzi sitini na wawili katika kila kidato. Mimi ninayasomesha masomo ya Historia na Geografia. Mula uliyopita, ulikuwa mula wa kwanza ambao wanafunzi waliopiga hatua katika masomo yao kuendelea na masomo katika kidato kinachofuata. Tanga janga la Korona lienee katika pande zote za nchi, kumekuwa na hali ya wasiwasi kote nchini. Mimi mwenyewe sijawa shuleni tangu mwezi wa Machi. Walimu wengi wameathiriwa na athari za virusi vya korona sanasana wale ambao wako kwenye shule ya kibinafsi. Imenibidi nielekeze nguvu na wakati wangu kupanda mimea kama miwa, sukuma wiki na mingineyo ili nikaweze kulisha familia yangu. Pia, nina darasa la saa mbili kwenye mtandao ambayo huwa na funza somo la historia kwenye nyakati ya kwanza na somo la geographia kwenye nyakati ya tatu. Kuna mazuri na mabaya ambayo yamekuja na virusi vya Korona. Mabaya ni kuwa kuna marafiki zangu ambao ni walimu wa shule za kibinafsi ambao wamepateza mlo wao kwa kuwa walipigwa kalamu na ‘wakubwa’ wao. Mazuri ni kuwa kumeshahidiwa maendeleo kwenye sekta ya masomo kwa kuwa walimu wengi wameanza kufunza kwenye mtandao.
 
[submitted on 7/25/2020]
 

Life in Quarantine: Witnessing Global Pandemic is an initiative sponsored by the Poetic Media Lab and the Center for Spatial and Textual Analysis at Stanford University.

Our Sponsors and Partners

Find Us!

Center for Spatial and Textual Analysis (CESTA),
Stanford University

Address:
4th floor, Wallenberg Hall (bldg. 160)
450 Jane Stanford Way
Stanford, CA 94305
Stanford Mail Code: 2055