O.K., 25, a security professional in Kampala, Uganda

Kazi yangu ni ya ulinzi. Ninafanya ulinzi katika bweni la wafunzi wa vyuo vya vikuu vilivyopo mjini Ruaraka. Sisi kama walinda lango, tumeathiri vilivyo. Tumelazimika kutumia vifaa vya kupima joto ya mwili kila saa mtu anapopita langoni ili kuhakikisha kuwa joto yao ya mwili haipiati kiwango cha thelathini na saba. Ijapokuwa kazi hiyo imeongezeka, hatujapata ongezeko katika mapato yetu. Kuna wenzanu tuliyiyopo nao awali amabao walipoteza kazi zao kwa sababu kampuni yetu inayotuajiri ilikuwa inashuhudia shida ya mapato kwa kuwa watu ambao wanaishi kwa nyumba ambayo tulikuwa tunalinda hawakuwa wanalipa ada ya nyumba. Imebidi tuzae mask kila wakati na tunapokuwa tunapima joto ya miili ya watu inatubidi tupime kando yao na si mbele yao kwa sababu kuna uwezekano kuwa mtu ambaye unampima anaweza kuwa na virusi vya korona na kwa wakati huo anaweza kukohoa.Hata kila wakati ninaporudi nyumbani kutoka makazini, mke wangu anahakikisha kuwa jambo la kwanza nilifanye kule nyumbani ni kutoa nguo yangu na kunawisha mikono yangu.
 
[submitted on 7/25/2020]
 

Life in Quarantine: Witnessing Global Pandemic is an initiative sponsored by the Poetic Media Lab and the Center for Spatial and Textual Analysis at Stanford University.

Our Sponsors and Partners

Find Us!

Center for Spatial and Textual Analysis (CESTA),
Stanford University

Address:
4th floor, Wallenberg Hall (bldg. 160)
450 Jane Stanford Way
Stanford, CA 94305
Stanford Mail Code: 2055