S.M., 27, a delivery driver in Dar es Salaam, Tanzania

Kazi yangu ni la kuendesha malori kutoka nchi za Afrika Mashariki. Sanasana naendesha katika taifa la Kenya na Tanzania. Mimi husafirisha bidhaa kadha wa kadhi kutoka bandari ya Mombasa hadi kwenye bara ya Afrika Mahariki au kutoka bandarini kule Dar es Salaam kurudi kenya. Kabla virusi vya korona keenea mipakani na kote ulimwenguni, ilikuwa ni rahisi sana kufanya biashara kati ya nchi hizo mbili ya Kenya na Tanzania. Kuvuka mipaka ya Kenya na Tanzania ilikuwa ni rahisi kama kumeza chakula ulikokwisha tafuniwani. Miezi kama minne tangu janga la korona lifanyike imekuwa vigumu kupita mipakani kuelekea nchi ya Kenya. Cha kushangaza ni kuwa hakujakuwa na kufungwa kwa nchi kwa Tanzania ila Kenya wamefunga nchi yao. Kwa hivyo, ni vigumu sana kuvuka nchi ya Kenya. Serikali ya Kenya wamejaza polisi katika mipakani kwa hivyo inaweza kuchukua takriban wiki mbili kupita mipakani kwa kuwa inabidi upimwe ili ukaweze kuingia katika nchi ya Kenya. Masharti ni kuwa ikiwa umeopimwa na ukapatikana kuwa una virusi vya Korona hauruhusiwi kuingia kwenye nchi ya Kenya. Hivyo basi tumeathirika sana ikiwa tuna bidhaa ambayo yana urahisi wa kuharibika kama vile nyama, maziwa na kadhalika. Athari hizo zimesababisha kuanguka kwa mapata yetu.
 
[submitted on 7/25/2020]

Life in Quarantine: Witnessing Global Pandemic is an initiative sponsored by the Poetic Media Lab and the Center for Spatial and Textual Analysis at Stanford University.

Our Sponsors and Partners

Find Us!

Center for Spatial and Textual Analysis (CESTA),
Stanford University

Address:
4th floor, Wallenberg Hall (bldg. 160)
450 Jane Stanford Way
Stanford, CA 94305
Stanford Mail Code: 2055