W.A., 21, a caretaker in Kisumu, Kenya

Maneno haya naandika kama mwakilishi wa nyanya yangu ambaye yuko kwenye malazi ya watu wakongwe ambao wanajulikana kama ‘senior citizens’. Nyanya yangu ana umri wa miaka tisini na tatu. Kwa kuwa amu na shangazi wangu walikuwa kazini kule mjini, tulionelea kuwa nyumbani pa watu wakongwe ungekuwa mahali mwafaka kwako. Mahali anapoishi nyanya yangu pamoja na watu wazee wengine ambao hawajiwezi inadhaminiwa na wasamaria wema. Vitu kama vile vyakula, malazi, maji, nguo, stima na pesa ndongo ya kujikimu yote yalikuwa yanatoka kwa kampuni mbalimbali. Kwa bahati mbaya, tangu athari za virusi vya Korona, biashara nyingi ambayo ilikuwa wadhamini wao wamepata hasari nyingi na mapato madogo.

Vitu kama chakula na mavazi hawapati tena siku hizi. Shida ni kuwa kuna watu wengi wakongwe ili chakula, maji na mavazi ni chache. Inakuwa vigumu kwa kuwa kuna wakati ambao kuna baadhi yao ambao wanalala njaa. Hii inahatarisha maisha yao kwa kuwa afya yao si nzuri na kwa hiyo wanahitaji kukinga miili yao kutoka kwa mngonjwa.

Juzi tu, kampuni ya Kenya power ambayo inasimamia usambazaji wa stima ilikata stima kwa kuwa watu hao wakongwe walikuwa na walikuwa na deni ya miezi ya kutolipa ada ya stima. Hivyo basi kwa siku mbili mtawalia watu hao wakongwe waliketi kwenye giza. Ni muhimu kukumbuka kuwa wazee hao wanahitaji joto ya stima ili wasiwe na baridi.

[submitted on 7/28/2020]

Life in Quarantine: Witnessing Global Pandemic is an initiative sponsored by the Poetic Media Lab and the Center for Spatial and Textual Analysis at Stanford University.

Our Sponsors and Partners

Find Us!

Center for Spatial and Textual Analysis (CESTA),
Stanford University

Address:
4th floor, Wallenberg Hall (bldg. 160)
450 Jane Stanford Way
Stanford, CA 94305
Stanford Mail Code: 2055