A.M., 19, a house cleaner in Thika, Kenya

Ninaishi kijijini Thika. Thika ni takriban kilomita ishirini na minne kutoka jiji la Nairobi. Njia ya kupata mlo na kulisha familia ni kupitia usafishaji. Mimi husafishia watu nguo, vyombo, watoto na sakafu. Kwa siku moja, ninaweza nikachukua masaa kumi kufanya kazi hizo. Kazi hiyo huhusisha kuuenda kwa nyumba za watu kwa kuwa ni mtu mmoja ninayemfulia nguo. Kwa kuwa hatuna vile vifaa vya kisasa vya kufulia nguo, mimi hutumia mikono kuzitekeleza kazi hizo. Hivyo basi, katika kile kisa cha kufulia nguo huwa kunafanyika mguso kati ya mikono na nguo zile. Tangu virusi vya Korona vienee kila mahali, watu wengi hawaajiri wajakazi ili wawafanyie kazi. Hiyo basi ni mgumu sana kwa wajakazi kama sisi kupata pato la kujikimu na familia yao. Kwa sasa, unapata kuwa watu wanajifulia nguo au wanapeleka wafuliwe kwenye vifaa vya kisasa vya kufulia nguo. Hii ni kwa kuwa watu hao wanaogopa kuwa mguso wa nguo zao utafanya uambukizo wa virusi vya Korona.
 
[submitted on 7/26/2020]
 

Life in Quarantine: Witnessing Global Pandemic is an initiative sponsored by the Poetic Media Lab and the Center for Spatial and Textual Analysis at Stanford University.

Our Sponsors and Partners

Find Us!

Center for Spatial and Textual Analysis (CESTA),
Stanford University

Address:
4th floor, Wallenberg Hall (bldg. 160)
450 Jane Stanford Way
Stanford, CA 94305
Stanford Mail Code: 2055